Author name: geraldwaniha@gmail.com

WAZIRI SIMBACHAWENE AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUTUMIA MIFUMO YA KIDIJITI KURAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amezitaka Taasisi zote za Umma kuhakikisha zinatumia mifumo katika kuwahudumia wananchi kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma bora, urahisi na haraka. Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati wa akifungua Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yenye kaulimbiu ya \”Himiza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji\”  Amesema Serikali imejenga mifumo mingi ikiwemo wa kufuatilia utendaji kazi wa watumishi ambao umeondoa ubabaishaji. Kadhalika, Waziri Simbachawene amewataka wananchi kutumia mfumo wa e-malalamiko na e-mrejesho ili kuweza kuainisha changamoto ambazo Serikali itazifanyia kazi kwa wakati na kuboresha utoaji wa huduma. \”Nizielekeze Taasisi zote za Umma kutumia mifumo iliyojengwa ili kurahisisha utoaji wa huduma bora, kwa haraka na kwa urahisi.\” Kwa upande wake Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma imeshirikisha Wizara 23, Mikoa 5, Halmashauri 3 na taasisi za umma 101 zimeshiriki. Amesema kupitia maadhimisho hayo wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja, kufahamu majukumu ya Taasisi na Wizara kupata mrejesho ili kuboresha utoaji wa huduma. Katika hatua nyingine, Bw. Mkomi ametoa wito kwa wananchi, watumishi wa umma na wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ambapo Maadhimisho hayo yataendelea hadi Juni 27 mwaka huu.

WAZIRI SIMBACHAWENE AZITAKA TAASISI ZA UMMA KUTUMIA MIFUMO YA KIDIJITI KURAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI Read More »

KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, ATOA SHUKRANI KWA USHIRIKI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametembelea mabanda ya Wizara na Taasisi za Umma ili kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hizo pamoja na kutoa shukrani kwa ushiriki mkubwa katika Maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025. “Ninapongeza na kutoa shukrani nyingi kwa Wizara na Taasisi zote za Umma zilizoshiriki katika Maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma, zimeonesha ushirikiano mkubwa na idadi ya ushiriki imekuwa kubwa,” amesema Bw. Mkomi Bw. Mkomi ameseongeza kuwa, kupitia maadhimisho hayo wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja, kufahamu majukumu ya Wizara na Taasisi pamoja na kupata mrejesho wa utendaji kazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma. Aidha, Katibu Mkuu Mkomi ameendelea kutoa wito kwa Watumishi wa Umma, Wananchi na Wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ili kupata huduma mbalimbali.

KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWENYE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, ATOA SHUKRANI KWA USHIRIKI Read More »

NAIBU WAZIRI SANGU APONGEZA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWA KUWA NA UTAYARI WA KUWAHUDUMIA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ametoa pongezi kwa Wizara na Taasisi za Umma kwa kuwa na utayari wa kuwahudumia watumishi wa umma na wananchi katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. “Tumekuwa tukifanya kliniki katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi wa Umma na Wananchi, lakini kupitia Maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamekuwa suluhisho kwa kufanya kazi papo kwa hapo kwani  Watumishi wa Umma na Wananchi wamekuja kuhudumiwa kwa wakati,hii inaonesha ni kwa namna gani mmekuwa na utayari wa kutoa huduma bora kwa maslahi ya taifa, hongereni sana,” Mhe. Sangu amesema Aidha, Mhe. Sangu ametoa rai kwa Watanzania wote kufika katika Viwanja hivyo ili kupata huduma za moja kwa moja na elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara na taasisi za Umma. Katika hatua nyingine, Mhe. Sangu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watumishi wa umma nchini kwa kuboresha maeneo yao ya kazi kwa kuwa sehemu salama ili watanzania waweze kupata huduma bora.

NAIBU WAZIRI SANGU APONGEZA WIZARA NA TAASISI ZA UMMA KWA KUWA NA UTAYARI WA KUWAHUDUMIA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA Read More »

WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA ATOA WIKI TANO TAASISI ZA SERIKALI KUJIUNGA NA MFUMO UNAOWEZESHA SERIKALI KUWASILIANA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza Taasisi za Serikali ambazo hazijajiunga na mfumo wa kielektroni utakaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana (GovESB) kujiunga na mfumo huo ifikapo Julai 30 mwaka huu ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Mhe. Majaliwa ametoa maagizo hayo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma. “Taasisi zote za umma ambazo hazijajiunga na mfumo huu mwisho ni Julai 30 mwaka huu, wote mhakikishe mmejiunga GovESB, huu ni msisitizo ambao ulitolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kila taasisi ipeleke mfumo wake eGA, idadi ya taasisi zilizounganishwa ni chache, hakuna gharama na hutakiwi kupanga bajeti” Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa mfumo huo unafaida kubwa katika utumishi wa umma kwani utasaidia kurahisisha utendaji, kutoa taarifa kwa wakati, kuondoa makosa ya kibinadamu katika kuwahudumia wananchi pamoja na kuwabana wala rushwa. “Nimefurahi kujulishwa kwamba jumla ya mifumo 223 kutoka kwenye taasisi 185 imeunganishwa na kusomana”. Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za umma zenye mifumo na zinazoendelea kubuni mifumo zihakikishe mifumo hiyo inasomana na inaweza kubadilishana taarifa kupitia mfumo huo wa GovESB ikiwa ni njia mojawapo ya kuendelea kuboresha huduma za Serikali. Kadhalika, Mhe. Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kuhakikisha mifumo iliyounganishwa inaendelea kubadilishana taarifa pamoja na kujiridhisha kwa kila anayeingia awe na uwezo wa kuwasiliana na wengine wote waliomo ndani. Katika hatua nyingine, Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa watumishi wa umma kuzingatia miiko na maadili ya utumishi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingitia Sera na Sheria kwa manufaa na maendeleo ya Taifa letu. “Nitumie nafasi hii kuwapongeza sana watumishi wote wa umma nchini, niwahikishie kuwa serikali ya awamu ya sita iko pamoja nanyi, fanyeni hivyo kwa ajili ya manufaa na maendeleo ya Taifa letu”, amesema Mhe. Majaliwa.  Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene amesema Tanzania imetambulika kimataifa ambapo mwaka 2022 Benki ya Dunia ilifanya utafiti kuhusu ukomavu wa matumizi ya teknolojia duniani katika utoaji wa huduma za Serikali na ushirikishwaji wa wananchi. Amefafanua kuwa ripoti ya utafiti huo iliyotolewa Machi, 2023 ilibanisha kuwa Tanzania imefanikiwa kupanda daraja kutoka kundi B hadi kundi A na kushika nafasi ya 26 duniani, nafasi ya 2 Afrika na nafasi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki. Katika tukio hilo, Mhe. Majaliwa amezindua mifumo miwili ambayo ni Mfumo wa kielektroni unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa ujulikanao kama Government Enterprises Service Bus (GovESB) pamoja na Mfumo wa e-Wekeza unaomuwezesha Mtumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida (Faida Fund). Siku ya Utumishi wa Umma husherehekewa Juni 23 kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla.

WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA ATOA WIKI TANO TAASISI ZA SERIKALI KUJIUNGA NA MFUMO UNAOWEZESHA SERIKALI KUWASILIANA Read More »

KATIBU MKUU MKOMI AWAASA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUJITATHMINI WANAPOTOA HUDUMA KWA UMMA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amewaasa watumishi wa ofisi hiyo kujitathmini wanapotoa huduma kwa umma wakiwemo Watumishi wa Umma kutoka katika taasisi mbalimbali, Wadau na Wananchi wanaohitaji kuhudumiwa kwenye masuala ya kiutumishi. Bw. Mkomi ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi yake katika eneo maalum la mafunzo kwa watumishi hao yanayofanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma. “Ofisi yetu inatoa huduma mbalimbali za kiutumishi, ninawaasa mjitathmini kwa namna mnavyotoa huduma kwa Watumishi wa Umma, Wadau na Wananchi ili tupate mrejesho mzuri kutoka kwao na hatimae kufikia malengo ya Serikali katika kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.” amesema Bw. Mkomi. Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo Balozi Omar Kashera amesema ni vizuri kuwa na uzalendo wa kujenga taswira nzuri ya ofisi kwa kuwa na viongozi bora, kufanya maamuzi sahihi kwa Watumishi wa Umma, Wadau na Wananchi wanaowahudumia ikiwa ni pamoja na kufikiri kwa kina, kushirikisha watumishi wanaofanya nao kazi ili kupata maamuzi jumuishi yatakayokuwa sahihi kwa maslahi ya Taifa.

KATIBU MKUU MKOMI AWAASA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUJITATHMINI WANAPOTOA HUDUMA KWA UMMA Read More »

Scroll to Top