Author name: geraldwaniha@gmail.com

UCHUMI WA TANZANIA WAENDELEA KUKUA – NAIBU WAZIRI SANGU ATOA ONYO KWA WATUMISHI WASIOWAJIBIKA

Uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023 hadi kufikia asilimia 5.5 mwaka 2024, hali inayoonesha mwelekeo mzuri wa maendeleo ifikapo mwaka 2030. Kauli hiyo imetolewa Julai 24, 2024 jijini Arusha na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Deus Clement Sangu (Mb), wakati akifunga rasmi Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Jumuiya ya Wataalamu wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala (TAPA-HR). Naibu Waziri Sangu alisema kuwa jitihada kubwa za serikali zimewezesha uchumi kuendelea kuimarika, na akasisitiza kuwa wataalamu wa rasilimali watu wana mchango mkubwa katika kuhakikisha watumishi wa umma wanasimamiwa ipasavyo kwa maendeleo ya taifa. \”Niwapongeze kwa kazi nzuri ya kusimamia watumishi wa umma, tumeona mabadiliko makubwa, lakini niwakumbushe kuwa kutowajibika kikamilifu kunaweza kuisababishia serikali hasara kubwa, alisema Sangu.Akitoa mfano, alieleza tukio la mwaka 2016 ambapo taasisi moja ya umma ilifukuza watumishi 40 bila kufuata taratibu, na baada ya kukata rufaa, mahakama iliamuru warejeshwe kazini na walipwe zaidi ya shilingi bilioni 40. \”Mtumishi mmoja anatakiwa alipwe zaidi ya bilioni moja, haya ni madhara ya mtu mmoja kutowajibika kazini, na sasa serikali inalazimika kulipa madeni badala ya kuendelea na miradi ya maendeleo, aliongeza Naibu Waziri.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAPA-HR, Bi. Grace Meshy, aliipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka sera bora zinazoboresha mazingira ya kazi na motisha kwa watumishi wa umma. \”Tunashukuru serikali kwa jitihada zake katika kuboresha sekta ya utumishi,tumeshuhudia mazingira bora ya kazi na ushirikiano mzuri baina ya serikali na wataalamu wa sekta hii, alisema Bi. Meshy. Aidha, aliwapongeza waajiri kwa kuruhusu zaidi ya washiriki 1,000 kuhudhuria mkutano huo, hatua inayoonesha kuthamini taaluma ya usimamizi wa rasilimali watu nchini.

UCHUMI WA TANZANIA WAENDELEA KUKUA – NAIBU WAZIRI SANGU ATOA ONYO KWA WATUMISHI WASIOWAJIBIKA Read More »

TAPA HR WATAKIWA KUUNDA BODI ILI KUPUNGUZA UKIUKWAJI WA MAADILI KAZINI

KATIBU Mkuu Kiongozi  wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said ameagiza  Jumuiya ya Wataalam wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Utumishi wa Umma (TAPA -HR) kuanzisha  mchakato wa uundwaji wa bodi ya taaluma kwa kada hiyo ili kuondoa sintofahamu  ya ukiukwaji wa maadili  na kuleta tija katika ufanisi wa kazi  Agizo hilo lilitolewa leo Jijini Arusha na Mhandisi  Zena Ahmed Said wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa (TAPA-HR) wenye kauli mbiu ya mwelekeo mpya wa nafasi ya w ataalamu wa Usimamizi wa Rasilimali Watt na Utawala :Kusukuma  Mabadiliko, Kuendana na Mageuzi na Teknolojia kwaajili ya kuboresha huduma katika Utumishi wa Umma unaofanyika kwa siku nne. Amesema  endapo bodi hiyo ikiundwa itaondoa malalamiko mengi ya ukiukwaji wa taaluma ikiwemo kukaa na Chuo cha Utumishi wa Umma ili kuwapa mahitaji ya kitaaluma ya  kada hiyo ili waweze kuhuisha na kuboresha maudhui na utaratibu wa kitaaluma wa kada ya maofisa rasilimali watu na maofisa utawala katika kuakisi mahitaji ya sasa kwamujibu wa miongozo iliyopo Alisema pia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kufanyia kazi hoja iliyowasilishwa kuhusu kuhuisha muundo wa utumishi kwa maendeleo ya kada hiyo ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sasa ikiwemo kuendana na kasi na ari katika ufanisi wa kazi \”Muundo uliopo  ni wa zamani  unatakiwa uhuishwe ili ulete tija zaidi lakini pia bodi hii itawasaidia kupata uhalisia wa nidhamu pamoja na kuondoa malalamiko kwa baadhi ya maofisa wanaokiuka kanuni na miongozo ya utumishi wa umma\” Alisema pia wasimamie wajibu na haki za watumishi pamoja na rasilimali zilizopo mahali pa kazi ikiwemo kushauri waajiri kujiunga na kutumia kikamilifu mifumo ya kidigiti ambayo imesanifiwa na ofisi ya Rais , menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ili kupunguza vitendo vya rushwa, kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi. Aliongeza kuwa watumishi waandaliwe ili kuendana na kasi ya mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kutokea katika taaluma zao ikiwemo mpango wa  mafunzo unaoendana na mpango wa taasisi za serikali katika utelezaji wa dira ya Taifa kwa mwaka 2025-2050 ikiwemo mpango wa kuridhishana madaraka ili kuondoa sintofahamu pale viongozi  wanapotaka kuteua watumishi wengine Naye Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi na Utawala Bora, Xavier Mrope  alisisitiza dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka2025/ 2050 iliyozunduliwa na Rais itasaidia wataalam hao kuleta tija zaidi na kusisitiza kubadilika kutokana mabadiliko ya teknolojia inayokua kwa kasi  zaidi.  Nate Mwenyekiti wa TAPA-HR,Grace Fransic amesema chama hicho kinalengo la ukuzaji wa taaluma zao lakini pia wanakabiliwa na changamoto waliyonayo ni changamoto ya muundo uliopitwa na wakati na kuiomba serikali kuboresha au kuhuisha muundo huo ili kuendana na mabadiliko ya sasa  Huku Katibu  Tawala Msaidizi Menejimenti ya Ufuatiliaji na Ukaguzi Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha,Ramadhani Madeleka kwaniaba ya Katibu Tawala Mkoa huo, Missaile  Mussa alishukuru mkutano huo kufanyika Jijini Arusha na Kong kuwa usalama katika mkoa huo umeimarika Mkutano huo umejumuisha washiriki zaidi ya 999 kutoka kada mbalimbali za maofisa rasilimali watu lakini pia walizindua tovuti ya Jumuiya hiyo pamoja na kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora.

TAPA HR WATAKIWA KUUNDA BODI ILI KUPUNGUZA UKIUKWAJI WA MAADILI KAZINI Read More »

WATAALAMU RASILIMALIWATU KUKUTANA ARUSHA 

Watumishi zaidi ya 700 kutoka kwenye taasisi mbalimbali za serikali wanatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kwanza wa Jumuiya ya Waalamu wa Usimamizi wa RasilimaliWatu na Utawala katika Utumishi wa Umma (TAPA-HR),utakaofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), 22 hadi 25 Julai,2025. Hayo yalisemwa jana jijini Arusha na Mwenyekiti wa TAPA-HR, Grace Meshy,wakati akizungumza na waandishi wa habari na alisema mkutano utafunguliwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Simbachawene. Alisema Jumuiya za Wataalamu hao,imeundwa kutekeleza malengo ikiwamo kuhakikisha kunakuwa na fursa ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala, kukuza ujuzi na weledi katika masuala ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala. Pia alisema wanajukumu la kuhifadhi na kusambaza taarifa za kitaaluma katika kada ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala kwa njia ya machapisho, mikutano, ziara za mafunzo,makongamano ya kitaaluma, midahalo na kuweza kujiunga na mitandao ya kitaaluma ya kitaifa na kimataifa. Mwenyekiti huyo,alisema malengo mengine ya kuundwa TAPA-HR  ni pamoja na kuimarisha maadili ya kitaaluma katika masuala ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala,kukuza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa kupitia mashirika na taasisi zinazojishughulisha na ukuaji na usimamiaji wa rasilimaliwatu na Kuimarisha utekelezaji wa mifumo inayotumika katika utumishi wa umma inayotumika katika usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala ili kufikisha huduma kwa umma na kuleta ustawi kwa umma. Hata hivyo,alisema mkutano huo, umelenga kuwakutanisha wataalamu wa kada ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala katika Utumishi wa Umma kutoka Tanzania bara na visiwani ili kuwajengea uwezo zaidi na kuongeza tija katika ufikiaji wa malengo makuu ya taasisi zao na ustawi wa wananchi kwa jumla. Alisema kamati ya maandalizi ya mkutano imeandaa mada mbalimbali zinazolenga kuimarisha utendaji kazi wa watumishi hao, na zitawasilishwa na wawezeshaji nguli katika utumishi wa umma ambao watapata nafasi ya kueleza uzoefu wao. Aidha amewaomba waajiri wote katika Wizara,Tawala za Mikoa Mamlaka ya Serikali za Mitaa,Wakala wa Serikali,Mashirika ya Umma,Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki,pamoja na Idara zinazojitegemea kuwawezesha Wataalamu wao wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala kushiriki katika mkutano huo mkuu wa kitaalamu ili waweze kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao mahala pa kazi.  

WATAALAMU RASILIMALIWATU KUKUTANA ARUSHA  Read More »

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo, Bi. Mary Mwakapenda wakati alipofika kukagua maendeleo ya maandalizi ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayotarajiwa kufanyika tarehe 17 Juni, 2025 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025 Read More »

KARIBU TUKUHUDUMIE: WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 inatoa huduma za kiutumishi katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2025. Hivyo, Watumishi wa Umma na Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la ofisi hiyo ili kupata huduma mbalimbali za kiutumishi. Baadhi ya huduma hizo ni Mifumo ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, e-Watumishi (HCMIS), e-Msawazo (HR-Assessment), e-Uhamisho (Watumishi Portal), e-      Mikopo, e-Utendaji, e-Likizo na e-Mrejesho.  Kadhalika, ofisi kwa kushirikiana na viongozi wengine watashughulikia masuala ya PEPMIS. Aidha katika banda hilo zitatolewa huduma nyingine mathalani huduma za kisheria katika Utumishi wa Umma

KARIBU TUKUHUDUMIE: WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025 Read More »

Scroll to Top