July 31, 2025

UCHUMI WA TANZANIA WAENDELEA KUKUA – NAIBU WAZIRI SANGU ATOA ONYO KWA WATUMISHI WASIOWAJIBIKA

Uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023 hadi kufikia asilimia 5.5 mwaka 2024, hali inayoonesha mwelekeo mzuri wa maendeleo ifikapo mwaka 2030. Kauli hiyo imetolewa Julai 24, 2024 jijini Arusha na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Deus Clement Sangu (Mb), wakati akifunga rasmi Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Jumuiya ya Wataalamu wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala (TAPA-HR). Naibu Waziri Sangu alisema kuwa jitihada kubwa za serikali zimewezesha uchumi kuendelea kuimarika, na akasisitiza kuwa wataalamu wa rasilimali watu wana mchango mkubwa katika kuhakikisha watumishi wa umma wanasimamiwa ipasavyo kwa maendeleo ya taifa. \”Niwapongeze kwa kazi nzuri ya kusimamia watumishi wa umma, tumeona mabadiliko makubwa, lakini niwakumbushe kuwa kutowajibika kikamilifu kunaweza kuisababishia serikali hasara kubwa, alisema Sangu.Akitoa mfano, alieleza tukio la mwaka 2016 ambapo taasisi moja ya umma ilifukuza watumishi 40 bila kufuata taratibu, na baada ya kukata rufaa, mahakama iliamuru warejeshwe kazini na walipwe zaidi ya shilingi bilioni 40. \”Mtumishi mmoja anatakiwa alipwe zaidi ya bilioni moja, haya ni madhara ya mtu mmoja kutowajibika kazini, na sasa serikali inalazimika kulipa madeni badala ya kuendelea na miradi ya maendeleo, aliongeza Naibu Waziri.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAPA-HR, Bi. Grace Meshy, aliipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka sera bora zinazoboresha mazingira ya kazi na motisha kwa watumishi wa umma. \”Tunashukuru serikali kwa jitihada zake katika kuboresha sekta ya utumishi,tumeshuhudia mazingira bora ya kazi na ushirikiano mzuri baina ya serikali na wataalamu wa sekta hii, alisema Bi. Meshy. Aidha, aliwapongeza waajiri kwa kuruhusu zaidi ya washiriki 1,000 kuhudhuria mkutano huo, hatua inayoonesha kuthamini taaluma ya usimamizi wa rasilimali watu nchini.

UCHUMI WA TANZANIA WAENDELEA KUKUA – NAIBU WAZIRI SANGU ATOA ONYO KWA WATUMISHI WASIOWAJIBIKA Read More »

TAPA HR WATAKIWA KUUNDA BODI ILI KUPUNGUZA UKIUKWAJI WA MAADILI KAZINI

KATIBU Mkuu Kiongozi  wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said ameagiza  Jumuiya ya Wataalam wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Utumishi wa Umma (TAPA -HR) kuanzisha  mchakato wa uundwaji wa bodi ya taaluma kwa kada hiyo ili kuondoa sintofahamu  ya ukiukwaji wa maadili  na kuleta tija katika ufanisi wa kazi  Agizo hilo lilitolewa leo Jijini Arusha na Mhandisi  Zena Ahmed Said wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa (TAPA-HR) wenye kauli mbiu ya mwelekeo mpya wa nafasi ya w ataalamu wa Usimamizi wa Rasilimali Watt na Utawala :Kusukuma  Mabadiliko, Kuendana na Mageuzi na Teknolojia kwaajili ya kuboresha huduma katika Utumishi wa Umma unaofanyika kwa siku nne. Amesema  endapo bodi hiyo ikiundwa itaondoa malalamiko mengi ya ukiukwaji wa taaluma ikiwemo kukaa na Chuo cha Utumishi wa Umma ili kuwapa mahitaji ya kitaaluma ya  kada hiyo ili waweze kuhuisha na kuboresha maudhui na utaratibu wa kitaaluma wa kada ya maofisa rasilimali watu na maofisa utawala katika kuakisi mahitaji ya sasa kwamujibu wa miongozo iliyopo Alisema pia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kufanyia kazi hoja iliyowasilishwa kuhusu kuhuisha muundo wa utumishi kwa maendeleo ya kada hiyo ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sasa ikiwemo kuendana na kasi na ari katika ufanisi wa kazi \”Muundo uliopo  ni wa zamani  unatakiwa uhuishwe ili ulete tija zaidi lakini pia bodi hii itawasaidia kupata uhalisia wa nidhamu pamoja na kuondoa malalamiko kwa baadhi ya maofisa wanaokiuka kanuni na miongozo ya utumishi wa umma\” Alisema pia wasimamie wajibu na haki za watumishi pamoja na rasilimali zilizopo mahali pa kazi ikiwemo kushauri waajiri kujiunga na kutumia kikamilifu mifumo ya kidigiti ambayo imesanifiwa na ofisi ya Rais , menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ili kupunguza vitendo vya rushwa, kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi. Aliongeza kuwa watumishi waandaliwe ili kuendana na kasi ya mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kutokea katika taaluma zao ikiwemo mpango wa  mafunzo unaoendana na mpango wa taasisi za serikali katika utelezaji wa dira ya Taifa kwa mwaka 2025-2050 ikiwemo mpango wa kuridhishana madaraka ili kuondoa sintofahamu pale viongozi  wanapotaka kuteua watumishi wengine Naye Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi na Utawala Bora, Xavier Mrope  alisisitiza dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka2025/ 2050 iliyozunduliwa na Rais itasaidia wataalam hao kuleta tija zaidi na kusisitiza kubadilika kutokana mabadiliko ya teknolojia inayokua kwa kasi  zaidi.  Nate Mwenyekiti wa TAPA-HR,Grace Fransic amesema chama hicho kinalengo la ukuzaji wa taaluma zao lakini pia wanakabiliwa na changamoto waliyonayo ni changamoto ya muundo uliopitwa na wakati na kuiomba serikali kuboresha au kuhuisha muundo huo ili kuendana na mabadiliko ya sasa  Huku Katibu  Tawala Msaidizi Menejimenti ya Ufuatiliaji na Ukaguzi Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha,Ramadhani Madeleka kwaniaba ya Katibu Tawala Mkoa huo, Missaile  Mussa alishukuru mkutano huo kufanyika Jijini Arusha na Kong kuwa usalama katika mkoa huo umeimarika Mkutano huo umejumuisha washiriki zaidi ya 999 kutoka kada mbalimbali za maofisa rasilimali watu lakini pia walizindua tovuti ya Jumuiya hiyo pamoja na kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora.

TAPA HR WATAKIWA KUUNDA BODI ILI KUPUNGUZA UKIUKWAJI WA MAADILI KAZINI Read More »

Scroll to Top